Wednesday, March 6, 2013

Wanaume wanatutumia




Hivi ni kweli kuwa tunatumiwa? Sio kwamba tunatumiana?





Hembu tusaidiane kuondoa hii zana ambayo kwangu mimi naona ni ya kizamani hasa ukitilia maanani swala la usawa ambao wanawake tumekuja juu kweli kweli karne hii.


Unapoanza uhusiano wa kimapenzi na mtu ni wazi kuwa mnakwenda ku-share kila kitu kuanzia pumzi, mapigo ya mioyo, mwili na ikikaa vema basi mpaka maswala la uchumi na kila kitu kinachohusu UHUSIANO wa KIMAPENZI.

Kwa wanawake wengi tunapokuwa ndani ya mahusiano na kwa bahati mbaya uhusiano huo ukafa kwa sababu zozote zile iwe ni mapungufu uliyoshindwa kuyavumilia au yeye kashindwa kuvumilia mapungufu yako n.k. utakuta jamii au mwanamke mwenyewe anadai kuwa "Hashim" alikuwa namtumia/ananitumia.


Kwanini basi isiwe "tulikuwa tunatumiana", manake kama ni swala la kufanya mapenzi nyote wawili mlifanya kwa kukubaliana na bila shaka nyote mkafurahia.


Ikiwa ni kusaidia shughuli za ndani au kiuchumi hiyo ilikuwa "choice" yako kwamba hukulazimishwa kufanya hivyo bali ulifanya kama sehemu ya mapenzi yako kwake......sasa swala la "alikuwa nanitumia" huwa linatoka wapi?


Nimejaribu kufanya uchunguzi wangu wa kienyeji na nimegundua kuwa hii inatokana na jamii ya wanawake kutegemea mambo fulani kutoka kwa mpenzi wa kiume na mambo hayo ya sipotimizwa basi anahisi "katumiwa".

No comments:

Post a Comment