Monday, February 25, 2013

Somo la mapenzi ambalo mwalimu wako hakukufundisha!


Hivi unajua kuwa watu tunatumia muda mwingi kufikiria kuhusu mahusiano? kwamba unatamani ungekuwa kwenye uhusiano ikiwa huna mwenza, ungekuwa nje ya uhusiano ulio nao kwa sasa kwa vile huna raha, ungebaki kwenye uhusiano uliouacha kwa sababu bado unampenda mpenzi wako au kuboresha uhusiano ulio nao ambao unaelekea kubaya.


Mahusiano yanachukua/gharimu sehemu kubwa sana ya muda na nguvu zetu, mahusiano ni muhimu ktk maisha yetu, mafanikio yetu, furaha/raha zenu. Mahusiano yanagusa kila kona ya maisha yetu kuanzia kazini, nyumbani, familia na mapenzi.

Uhusiano wenyewe unamaana kuwepo pale kwa ajili ya mwenzio, kuchangia na kusheherekea undani wa furaha ya ajabu na ya kipekee mioyoni mwetu (nani anataka kuwa mpweke jamani eeeh?).


Nyumbani na kwenye familia uhusaino unamaana kufurahia ukuaji wenu, ukaribu wenu, kupena matumaini, kukosoana, kurekebishana, ushirikiano wenu n.k.


Kazini/Shuleni uhusiano unamaana kusaidiana, kurekebishana, kupena matumaini, kukosoana, kupongezana yanapookea mafanikio n.k.
Kwenye mapenzi uhusiano unamaana kusheherekea “u-mutual”(nipe- nikupe), kupeana mapenzi yasio na kikomo, kushirikiana kila kitu kuanzia mate mpaka miili yetu, kukosoana, saidiana, rekebishana, jifunza n.k.


Kitu kinachonigusa kuhusu mahusiano ni kuwa hatukufundishwa tulipokuwa shuleni japo kuwa tulihitaji sana kujua jinsi ya kuanzisha uhusiano mzuri na wakudumu kwa muda mrefu ktk maisha yetu, yaani kama vile tulivyofundishwa Kiingereza, Hisabati, Historia, Sayansi, Sanaa na Michezo (well wangefundishaje wakati wao wenyewe hawajui).


*Kwenye somo la lugha ya Kiingereza kuna neno "Elation" ambalo linamaanisha furaha na ni mzizi wa kile ninachokizungumza hapa ambacho ni uhusiano (rELATIONship).


*Kwenye somo la Hisabati tulijifuza “Eros Equation”….unakumbuka? Sasa basi maana nyingine ya neno Eros ni upendo/mapenzi, na mapenzi ndio kiungo kikubwa cha mahusiano yetu. Ngoja nikupe mfano wa somo hili ambalo nilikuwa sio mzuri sana,

Find solution;
Tukio(mapungufu yake)+Unalichukuliaje (unafikiria nini cha kufanya)= Suluhisho (uzoefu wako, mapenzi yako, uoga na furaha yako).


Hapa unachotakiwa kufanya ni kutafuta suluhisho kwa kutumia kanuni ya MAGAZIJUTO…..Ondoa mabano, gawanya, zidisha, jumlisha kisha toa…ili uweze kufurahia uhusiano wako na kuongeza mapenzi kwa mpenzi wako.


Nitakuja kumalizia swala la uhusiano kwenye somo la Historia, Sayansi, Michezo na Sanaa.....sinauhakika na somo la siasa.


Nakutakiwa mwanzoo mwema wa wiki.

No comments:

Post a Comment